WAKULIMA MKOANI DODOMA WASHAURIWA KULIMA MAZAO YANAYOHIMILI UKAME

Na Hamida Ramadhani-Dodoma KATIKA kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi wakulima wa Mkoa wa Dodoma wameshauriwa kuendelea kulima mazao yanayostahimili ukame  ikiwemo  zao la Mtama na Uwele. Wito huo umetolewa jiji hapa na Meneja Mradi wa Kilimo   hifadhi kutoka Dayosisi ya Central Tanganyika DCT Busela Yuga alipotembelewa kwenye Bada lao la Kilimo